Mwanaume mmoja mkazi wa Mkoa wa Pwani Mombasa anayejulikana kama David Charo ‘ameponea chupuchupu’ baada ya kumeza mswaki kimakosa na ukakaa tumboni kwa takriban wiki moja hadi madaktari walipofanikiwa kuutoa.
Inaelezwa kuwa Charo alikuwa anapiga mswaki Jumapili wiki iliyopita apokuwa anajiandaa kwenda kazini Bamba, Kilifi ambapo mswaki huo ulikwama kwenye koo lake na baadae kutumbukia tumboni.
Madaktari katika Hospitali Kuu ya Mkoa ya Pwani (CPGH) mjini Mombasa, Kenya wamefanikiwa kuutoa mswaki huo kwa upasuaji wa kutumia matundu madogo.
Awali madaktari hao walisema wangeutoa mswaki huo kwa njia ya upasuaji. Hatahivyo inaelezwa kuwa tayari mwanaume huyo alikuwa ameanza kupata shida kwenye kupumua kutokana na mswaki huo.
Tsunami kubwa kuwahi kutokea duniani