Kutoka nchini Kenya, jana April 8, 2018, mtoto wa Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, Jomo Kenyatta alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Fiona Achola Ngobi.
Inaelezwa kuwa harusi ilifanyika Ikulu ya Rais na ilihusisha wageni wachache ambao ni ndugu na jamaa wa karibu wa familia hizo, huku sare ya harusi ikiwa ni wote kuvaa nguo za rangi nyeupe.
Harusi hiyo imefanywa kuwa private, ili kuepuka vyombo vya habari jambo ambalo limewezekana kwani hadi sasa hakuna picha zilizoonekana popote katika mitandao za harusi hiyo.
Wageni waalikwa hawakuruhusiwa kuingia kwenye harusi hiyo na simu wala kamera.
Achola ni mpwa wa aliyewahi kuwa Katibu wa Wizara ya Ulinzi Raychelle Omamo na mjukuu wa marehemu William Odongo Omamo ambaye amewahi kuwa Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mazingira na Maliasili na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Muhoroni.
Wawili hao Achola na Kenyatta walipata mtoto wao wa kwanza Wanjiru, November 2018.
Hifadhi ya Saanane Mwanza, imekuja na mbinu mpya kuvutia Utalii.