Kocha wa club ya Man City Pep Guardiola ametangaza kuwa na wasiwasi wapinzani wao Liverpool atakaocheza nao mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA, kufuatia kikosi chake kupoteza mechi mbili kwa jumla ya magoli sita katika kipindi cha siku nne.
Guardiola ametangaza kuwa kufuatia timu yake kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Man United ikitokea nyuma na baadae kupata ushindi wa magoli 3-2 katika uwanja wao wa Etihad na kupoteza mchezo wa kwanza wa UEFA Champions League ugenini dhidi ya Liverpool kwa magoli 3-0, amekiri kuanza kuwa na wasiwasi wa uwezo wa wachezaji wake katika mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool.
“Ndio imeleta ugumu zaidi hasa baada ya kushindwa kushinda derby na wapinzani wetu inashusha morali ya timu, kama tungekuwa tumepata walau goli mbili katika mchezo dhidi ya Liverpool ingeweza kusaidia kuongeza morali za wachezaji, kama tungecheza kama tulivyocheza kipindi cha kwanza ingeweza kufunga milango ya wapinzani kutufunga”>>> Pep Guardiola
Man City kupoteza kwa magoli 3-2 dhidi ya Man United katika uwanja wao wa nyumbani katika mchezo huo wa derby, Man City anakuwa kapoteza mchezo wake wa kwanza wa EPL nyumbani baada ya miezi 16 kupita, hivyo kufungwa kwa mechi ya EPL dhidi ya Man United na kufungwa na Liverpool katika champions League kumeichanganya Man City na kuhofia wachezaji wake wanaweza kufanya vibaya game zinazofuata kwa hofu.
VIDEO: Canavaro baada ya game amezungumzia ishu ya kustaafu