Mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameilalamikia Serikali Bungeni kwamba imekuwa ikiwasaliti wananchi wa mikoa ya kusini ikiwemo Lindi na Mtwara kwa kushindwa kuwasaidia katika kuboresha kilimo cha korosho na mbaazi na kusababisha hali mbaya ya kiuchumi kwa wakulima wa mazao hayo ikiwa wakati wa kampeni moja ya ushawishi wao ilikuwa ni kuwasaidia wakulima hao.
Nape amesema…>>>“Ukiacha gesi na mafuta, Lindi na mtwara ni korosho lakini Serikali ilichukua mfuko wa pembejeo. Kulikuw ana mapungufu yalitokea tukaacha kwakuwa ilikuwa ni mara ya kwanza lakini hali ilivyo sasa ni mbaya sana sana ”
“Tumaini pekee lililokuwa limebaki kusini ni korosho, mnajua mbaazi imekwenda kutoka Shilingi 2000 hadi 100 jamani sio sawa kabisa. Mnataka tuende wapi? Tulipotoa kura tuliamini mtatusaidia lakini imekuwa tofauti” –Nape Nnauye
Agizo la Serikali kuwarudisha kazini watumishi waliofukuzwa