Leo April 10, 2018 Stori niliyoipokea ni kuhusu Mabehewa manne ya Treni ya mizigo iliyokuwa inatoka Katavi kuelekea Tabora yameacha njia na kuanguka katika eneo la Shankala mkoani Katavi.
Afisa Uhusiano Shirika la Reli Mohamed Mapondela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo nakusema hakuna mtu alijeruhiwa wala uharibifu wa mali na kinachoendelea sasa ni kutoa mizigo na kuweka sawa njia ya treni ili safari iendelee.