Kutoka nchini Kenya katika Jimbo la Murang’a mtoto mmoja wa kike ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la tano, amebakwa na kisha kunyongwa na mwili wake kufichwa chini ya kitanda na mvulana wa kidato cha kwanza.
Binti huyo wa miaka 12 ambaye ni mkazi wa kijiji cha Gathuumbi alikuwa anasoma kwenye shule moja kijijini hapo.
Baada ya wanakijiji kugundua mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye ndiye mvulana huyo wa kidato cha kwanza walimpiga hadi kufa.
Baba mzazi wa marehemu binti huyo, Josephat Chege ameibua hisia nyingi baada ya kulia kwa muda mrefu bila kunyamaza huku akiliomba Jeshi la Polisi kuwalinda watoto kwa binti yake hakustahili kutendewa vile.
Rais Magufuli ametimiza ahadi, katoa mifuko 300 ya cement