Kocha wa Yanga George Lwandamina imeripotiwa kuwa yupo mbioni kuiacha club hiyo na kurejea kwao Zambia kuungana na club yake ya zamani ya Zesco United.
Stori kwa mujibu wa mtandao wa zambiafootball.co.zm umeripoti kuwa club ya Zesco imesaini mkataba wa awali na Lwandamina na inatarajia kumtangaza kuwa kocha wao mkuu muda wowote kutokea sasa na ataungana na timu mwezi May.
Inaripotiwa kuwa mkataba wa Yanga na Lwandamina unamalizika mwishoni mwa mwezi May na hakuna makubaliano yaliofikiwa ya kuongeza mkataba, hivyo Lwandamina amepokea ofa ya kurudi club yake ya zamani kwa mikono miwili.
Kama Yanga na Lwandamina watafikia makubaliano ya mapema zaidi kocha huyo anaweza kuungana na Zesco hata kabla ya mwezi May.
VIDEO: Canavaro baada ya game amezungumzia ishu ya kustaafu