Utafiti mpya umeonesha kuwa baada ya kuacha kuvuta sigara, ulaji wa nyanya mbichi na apple unaweza kusaidia kurekebisha uwezo wa mapafu.
Katika utafiti uliofanyika kwa miaka kumi, watafiti wamefanya upimaji wa uwezo wa mapafu na uchunguzi wa chakula kati ya watu zaidi ya 650 kutoka Ujerumani, Norway na Uingereza. Matokeo yameonesha kuwa, baada ya kuacha uvutaji wa sigara, ulaji wa nyanya na apple unaweza kupunguza athari kwenye mapafu.
Ukilinganisha watu wanaokula nyanya isiyozidi moja au matunda kwa siku, watu wanaokula nyanya zaidi ya mbili au matunda matatu, uwezo wa mapafu unaweza kupungua kwa kasi ndogo.
Utafiti umeonesha kuwa chakula hicho kinaweza kusaidia kurekebisha athari zinazotokana na uvutaji wa sigara. Wamesisitiza kuwa njia ya kula ni muhimu sana, ulaji wa nyanya na matunda unaweza kulinda mapafu.