Marais wawili wa zamani wa nchi ya Comoro wanashutumiwa kuhusika na ubadhirifu wa mamilioni ya Dola za Marekani kwa kuuza passport kwa wageni wa mataifa mawili ya Ghuba, na fedha hizo kutumika kugharamia miradi ya maendeleo.
Inaelezwa kuwa Bunge la nchi hiyo limeiomba mahakama ishughulikie kesi hiyo na kuwachukulia hatua viongozi hao wastaafu kama watakutwa na hatia hiyo.
Kashfa hiyo ilianza mwaka 2008 wakati Comoro ilipoanzisha mpango kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu na Kuwait, kuwapa uraia wakazi wa falme hizo mbili za Ghuba wa jamii ya Mabedui ambao hawakuwa wanatambuliwa kuwa na uraia wa nchi yoyote.
Hakimu aagiza Vyombo Serikali kuheshimiana katika kazi