Leo April 11, 2018 stori ninayokusogezea ni kutoka nchini Kenya ambapo Rais Uhuru Kenyatta amesaini muswada ambao sasa utakuwa sheria kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike nchini humo.
Kenyatta amesaini sheria hiyo April 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.
Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016 imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na kukosa pedi za kujistiri.