Ikiwa Umoja wa Mataifa leo April 13, 2018 ukifanya mkutano maalumu mjini Geneva Uswizi kuchangisha fedha za kukabiliana na janga la kibinadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, nchi hiyo imesusa kutokea kwenye mkutano huo.
Serikali ya DRC imekataa kuhudhuria mkutano huo na kueleza kuwa Umoja wa Mataifa kupitia mkutano wake huo wa kuifadhili DRC inafanya hali nchini hiyo ionekane mbaya ikiwa ni tofauti na uhalisia.
Umoja wa Mataifa umesema umeitisha mkutano huo ili kuchangia Dola za Marekani bilioni 1.7 sawa Shilingi za Kitanzania trilioni 4.08 kwa ajili ya kusaidia DRC.
DRC wamelaumu Umoja wa Mataifa kwa madai kuwa imetilia chumvi hali halisi iliyopo nchini humo na ukubwa wa tatizo lililopo.
Katibu Mkuu CHADEMA amezungumza Bulaya kushikiliwa Polisi