Ukatili wa kikundi cha wanaume kumbaka na kisha kumuua mtoto wa kike wa miaka 8 nchini India umesababisha hasira kali nchini humo na vurugu nchi nzima.
Mwili wa Asifa Bano ambaye alikuwa ni Muislamu wa kabila la wafugaji, ulikutwa msituni January 17 karibu na Mji wa Kathua katika Jimbo la Kashmir.
Mpaka sasa waliokamatwa na polisi ni pamoja na afisa wa mstaafu wa serikali, maafisa wa polisi wanne na mtoto mmoja, wote wakiwa ni wa jamii ya Hindu ambayo imehusishwa na mgogoro wa ardhi na wajumbe wa Kiislam.
Vurugu zimezidi baada ya mawaziri wawili kutoka chama cha Wahindu BJP kuhudhuria mgomo wa kuwaunga mkono wanaume hao wanaoshutumiwa kufanya uhalifu huo.
Mtoto 1 kati ya 1000 upata ugonjwa wa kupinda miguu, Wataalmu wanaelezea tiba