Utafiti mpya uliotolewa siku za hivi karibuni unaeleza kuwa kunywa pombe hata kwa kiwango cha chupa moja tu kwa siku hufupisha maisha ya mnywaji.
Wanasayansi wa utafiti huu walilenga kukosoa mawazo kuwa kunywa pombe kidogo hakuna madhara yoyote kiafya jambo ambalo linatajwa kuwa si la kweli.
Utafiti huu ambao ulifanywa kwa wanywaji pombe 600,000 umegundua kuwa kunywa vinywaji vyenye vilevi kati ya vitano hadi 10 kwa wiki hupunguza maisha ya mtu kwa miezi sita.
Pia inaeleza kuwa kwa wale wanaokunywa pombe kwa kiwango cha chupa 18 kwa wiki kupoteza hadi miaka mitano ya maisha yao.
Adhabu itakayokukuta usipochukua Risiti Petro Station