Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-PESA imetambuliwa na kupatiwa cheti kwa kutambua ubora uliotukuka wa huduma za kifedha. Tuzo hiyo imetolewa April 13, 2018 Abidjan, Côte d’Ivoire kutambua usalama na uhakika pamoja na nia thabiti ya M-Pesa katika kulinda haki ya mteja.
Tuzo hiyo imetolewa baada ya Vodacom Mpesa kufikia vigezo vilivyowekwa na GSMA ambavyo ni viwango vya juu vya kulinda amana ya mteja, usalama wa huduma, usiri na kulinda taarifa za mteja, kupambana na utakatishaji fedha, kupambana na wanaogharamia vikundi vya ugaidi, pia kupambana na mbinu zote za udanganyifu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Ian Ferrao, amesema “Utambuzi na cheti hiki vinathibitisha nia na utendaji wa Vodacom Tanzania katika kuhudumia na kulinda haki za mteja katika eneo lote la biashara ya MPesa,”
“Tukiwa ni mtandao unaoongoza kwa huduma ya pesa cheti hiki kitatupatia nafasi ya kuaminika zaidi na kutuongezea ari ya kiutendaji ili kuwaridhisha wateja wetu ambao wametufanya kuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini kupata utambulisho huu baada ya kufikia vigezo,” -Ian Ferrao
Cheti hiki cha GSMA kimekuja wakati ambapo Vodacom Mpesa inatimiza miaka 10 ya M-pesa Tanzania. Kwa takribani miaka 10 sasa M-pesa imeweza kubadilisha maisha na kuipandisha Tanzania kiuchumi kupitia huduma za kutuma na kutoa fedha, malipo ya bili, akaunti za kutunza fedha, mikopo na mengineyo mengi.
M-pesa leo ina zaidi ya wateja Milioni 8, wakala 106,000, biashara za kawaida zaidi ya 2000, wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 15,000, benki zilizounganishwa zaidi ya 30. Kupitia huduma zake M-pesa imewezesha wakazi wa kitanzania wa mijini na vijijini kuwa sehemu ya mfumo mzima wa kiuchumi unaotambulika, pamoja na ongezeko kubwa la kiuchumi katika jamii nyingi za kitanzania.
Mfumo huu rasmi nchini Tanzania umekuza uchumi kwa mwaka 2017 hadi kufikia 65% kutokea 58% mwaka 2013 na 44% kwa mwaka 2009 Mwaka mmoja baada ya M-pesa kufunguliwa rasmi nchini Tanzania.
MAGAZETI LIVE: Hofu Bungeni, Kashfa Nzito, Kimewaka