Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF jana April 13, 2018 limetoa ripoti iliyoeleza kuwa wapiganaji wa Kiislamu kutoka kundi la Boko Haram nchini Nigeria wameteka zaidi ya watoto ya 1,000 tangu mwaka 2013.
Wapiganaji hao wanaripotiwa kuteka vijana na kueneza hofu. Hayo yalisemwa katika maadhimisho ya miaka minne ya kutekwa kwa wasichana wa shule 276 kutoka mji wa Chibok.
Inaelezwa kuwa kuna uwezekano kuwa waliotekwa ni wengi zaidi ya idadi inayofikiriwa na hata wasichana waliotekwa na kuachiwa huru wameeleza kulazimishwa kuolewa na hata kubakwa na wapiganaji hao.
Binti mwenye ugonjwa wa kutonenepa