Mahakama ya Uhalifu Jijini Vienna nchini Austria imemhukumu kijana wa miaka 19 kifungo cha miaka tisa jela baada ya kumkuta na hatia ya kuhusika na mpango wa mashambulio mawili ya Kiislamu nchini Ujerumani.
Kesi hii imeonesha kuongezeka kwa changamoto ya vijana kuamua kujihusisha na vitendo vya ugaidi ndani na nje ya nchi zao.
Kijana huyo amegundulika kumshawishi mtoto wa kiume wa miaka 12 ambaye ni raia wa Ujerumani na Iraq, kutekeleza shambulio la kigaidi siku ya Krismasi katika soko lililopo mjini Ludwigshafen.
Katika kesi hiyo kijana huyo alikiri kuwa mwanachama wa kikundi cha kigaidi cha Islamic State na hata baada ya kuhukumiwa miaka 9 jela alisema kwa nguvu kuwa ‘sijali’.
Kilichojadiliwa Bungeni leo kuhusu mtoto Anthony Petro