Club ya Singida United inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kufanikiwa kupata udhamini na kampuni ya mbolea ya Yara, jitihada zake zimeanza kuoneka kutokana na wachezaji wake kuanza kujihusisha na kilimo.
Golikipa wao Said Lubawa ni miongoni mwa wachezaji wa Singida United wanaomiliki mashamba baada ya kupewa elimu ya kilimo na Yara, leo amefika nyumbani kwao mkoa wa Pwani na wachezaji wenzake kuwaonesha shamba lake.
Lubawa aliambatana na wachezaji wenzake Msingida pamoja na Msonjo kwa ajili ya kuwaonesha shamba lake analofanya nje ya soka, Lubawa sio staa wa kwanza wa Singida United kuhisisha na kilimo wapo pia wakiwa Deus Kaseke na Nizar Khalfan ambao wanamiliki mashamba ya mahindi.
ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1
https://youtu.be/-X6tg5a15HI