Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad kutoa taarifa ya mwaka ambayo iliibua mambo mbalimbali na baadae baadhi ya Mawaziri kuonekana wakiitasha mikutano na Waandishi wa habari kwa ajili ya kutolea ufafanuzi wa hoja za CAG Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ametoa onyo kwa wahusika.
“Zoezi linaloendelea hivi sasa kwa baadhi ya Mawaziri kutoa majibu ya hoja za CAG ni kinyume cha sheria , Sheria ya ukaguzi wa umma kifungu cha 38 (1), (2) kinaeleza utaratibu wa namna ambavyo hoja za ukaguzi zinapaswa kujibiwa na Mawaziri hawatajwi kabisa katika kifungu hicho” –Zitto Kabwe
“Wanaopaswa kujibu ni Makatibu wakuu wa Wizara na sio kujibu kwa kuita mikutano na Waandishi wa habari, hiki kinachofanyika na Mawaziri ni kinyume cha sheria na sheria imeweka adhabu kwa makosa hayo ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili jela au faini ya Shilingi Milioni tano” –Zitto Kabwe
Kilichojadiliwa Bungeni leo kuhusu mtoto Anthony Petro