Leo April 15, 2018 Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mohammed Mtonga amesema kuna tatizo la vihatarishi serikalini hasa kwa kutofikia malengo yaliyopo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahafari ya Taaasisi ya Kudhibiti Vihatarishi nchini (IRMT) Mtonga amesema vihatarishi ni hali ya kutofikiwa kwa malengo yaliyopo.
Mtonga amesema masuala ya vihatarishi awali yalikuwa yanagusa sekta ya Biashara na Benki lakini kwa sasa vinagusa hadi sekta za umma.
Amesema kuwa Serikali ilishatoa muongozo kuhusu suala hilo hasa kwa upande wa vihatarishi vya ubadhirifu.
“Hivyo tunategemea siku za usoni tukapata watu wengi sana wanaohitimu katika eneo la vihatarishi hasa katika uchumi wa viwanda,” -Mtonga
“Kwa upande wa serikali vihatarishi vipo hasa kwa kutofikia malengo yaliyopo, kwani vihatarishi vinafanya usifikie malengo,” -Mtonga
Video ya Nandy na Bilnass Mkuu wa Wilaya ametoa ushauri kwa Mastaa