Ilitoka ripoti kuwa ndege hiyo ilikuwa na watu 103 lakini maafisa wa ulinzi walitangaza tena kwamba ilikuwa na watu 78.
Ajali hiyo ambayo mtu mmoja tu ndiyo amenusurika na anapata matibabu ya majeraha hospitali hivi sasa wakati wengine wote wamefariki.
Ndege ya kijeshi aina ya Hercules C-130 ya Algeria ilikuwa na familia za wanajeshi wakielekea mji wa Costantine lakini ilipofika kwenye milima ya Oum al-Bouaghi kutokana na hali mbaya ya hewa ikapata ajali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na wizara ya ulinzi imesema kuwa hali mbaya ya anga iliyohusisha kimbunga na mvua kubwa ya barafu ilisababisha ajali hiyo.
Serikali ya Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo.