Michezo ya Play offs ya Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea leo Jumanne ya April 17 kwa michezo minne kuchezwa, club ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilikuwa ugenini kucheza mchezo wake wa nne wa Playoffs dhidi ya wenyeji wao KAA Gent katika uwanja wa GHELAMCO.
Kama kawaida kocha wa KRC Genk ameendelea kumuamini nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta na kumpanga katika kikosi cha kwanza cha Genk, Samatta katika mchezo huo uliyomalizika kwa sare tasa 0-0, alifanikiwa kucheza kwa dakika 65 pekee ndio kocha akafanya mabadiliko na kumuingiza mgiriki Nikolaos Karelis.
Kwa matokeo hayo sasa KRC Genk wanakuwa nafasi ya 5 katika timu sita zinazoshiriki michezo ya Playoffs, hivyo KRC Genk ili wapate nafasi ya Europa League moja kwa moja 2018/2019 wanapaswa wamalize game za playoffs wakiwa nafasi ya tatu ila wakiwa nafasi ya nne wataanzia game za playoffs za Europa League, Mbwana Samatta aliwahi kukiri kuwa na hamu ya kucheza michuano hiyo kwa mara ya pili.
ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1
https://youtu.be/-X6tg5a15HI