Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na club ya Real Madrid ya Hispania Ricardo Kaka ameamua kufunguka kuhusiana na maisha yake ya soka aliyowahi kukutana nayo akiwa Real Madrid chini ya kocha wa kireno Jose Mourinho.
Kaka ambaye ni mwaka mmoja sasa umepita toka atangaze kustaafu soka la ushindani licha ya kuwa alikuwa na misimu mizuri AC Milan kiasi cha kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or amekiri kuwa maisha yake kisoka chini ya Mourinho hayakuwa mazuri.
“Mwaka 2009 nilikubali ombi la Real Madrid la kujiunga nao lakini niliharibikiwa kisoka kukubali ombi hilo kwa maana nilishindwa kutoa nilichokuwa natoa Milan kisoka nilipotea, Mourinho namuheshimu lakini naweza kusema alikuwa kocha mgumu kwangu kuwahi kunifundisha na tulikuwa na mahusiano magumu”>>> Ricardo Kaka.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Kaka alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea AC Milan ya Italia kwa dau la pound milioni 56 lakini mwaka 2010 aliwasili Jose Mourinho na kuanza kazi hadi mwaka 2013, Kaka hadi anaondoka Real Madrid mwaka na kurudi AC Milan hakuwahi kufanya vizuri sana Real Madrid.
ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1
https://youtu.be/-X6tg5a15HI