Viongozi wa ngazi za juu nchini Cuba wamepiga kura rasmi na kufanya mkutano wa kitaifa wa kuidhinisha kuteuliwa kwa Miguel Díaz-Canel kuiongoza nchini hiyo.
Miguel ambaye ana umri wa miaka 55 mwenye taaluma ya Uhandisi anatarajiwa kuanza kuongoza taifa hilo leo na kuweka ukomo wa utawala miaka 60 ya familia ya Castro.
Kiongozi huyu anachukua nafasi ya Raul Castro ambaye ni ndugu wa kiongozi ambaye aliongoza mapinduzi ya mwaka 1959 ya nchi hiyo na kuendelea kuongoza hadi alipomwachia kijiti ndugu yake Raul Castro.
Chakufahamu kuhusu watu wenye macho ya BLUE na KIJANI