Kutoka nchini Burundi, Bunge la nchi hiyo limepitisha muswada wa sheria kuruhusu polisi kufanya ukaguzi katika makazi ya watu wa nchi hiyo bila kuwa na kibali maalumu.
Hatahivyo hatua hiyo imekosolewa na wabunge wa upinzani na watetezi wa haki za binadamu nchini humo.
Muswada huo umepitishwa na wabunge 97 na kupingwa na sauti 22 za wabunge wa upande wa upinzani.
Waziri wa Sheria nchini humo Aimé Laurentine Kanyana ameeleza kuwa sheria hiyo mpya itasaidia katika kupambana na visa vya mauaji ya kikatili, ugaidi, biashara ya kusafirisha binadamu na kumiliki silaha kinyume cha sheria, utumiaji wa dawa za kulevya pamoja na ubakaji.
BREAKING: CHADEMA wanaongea na Waandishi wa Habari