Aliyekuwa mkuu wa FBI nchini Marekani, James Comey amelieleza shirika la utangazaji la BBC kuwa haamini kama kuna kiongozi yeyote wa karibu wa Rais Donald Trump anayeweza kubadilisha tabia yake.
Comey akizungumza katika kipindi cha Newsnight amedai kuwa tabia za Trump zinahatarisha hadhi ya nchi na zinaathiri wale wanaomzunguka.
Ameeleza kuwa Rais Trump ana tabia ya kuongea uongo na kuwalazimisha wafuasi wake kumuunga mkono na kuamini anachokisema.
BREAKING: CHADEMA wanaongea na Waandishi wa Habari