Baada ya headlines za muda mrefu kuhusiana na vitendo vya ujangili kukithiri nchini Tanzania, mbinu mbalimbali wizara ya maliasili na utalii imekuwa izitumia ikiwemo kuongeza idadi ya askari katika hifadhi za taifa.
Kampuni ya uwindaji ya Otterlo Business Corporation Limited (OBC) ya Loliondo imekabidhi magari 15 kwa wizara ya maliasili na Utalii kwa ajili ya kusaidia kulinda rasilimali ya wanyamapori nchini.
Magari 15 yaliokabidhiwa na mkurugenzi msaidizi wa OBC Molloimet Yohana ni aina ya Toyota Landcruiser na thamani yake imetajwa kufikia Tsh Bilioni 1.5 lengo likiwa ni kusaidia askari kufanya doria.
“Sitaki kuona Askari ana kitambi, Kamishna akiapishwa ahakikishe hili” Dr. Kigwangalla