Mataifa ya Afrika katika historia hayawahi kutwaa Kombe la Dunia hata mara moja, hivyo Rais wa shirikisho la soka Nigeria (NFF) Amaju Pinnick amezichukua headlines baada ya kutangaza ahadi nono kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria watakaoshiriki World Cup 2018.
Amaju Pinnick ametangaza kuwa kama Nigeria watafanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Dunia na kutwaa taji hilo basi wachezaji watapata dola milioni 24 wagawane kama ambavyo walikubaliana awali, lengo likiwa ni motisha ya wao kufanya vizuri mwaka huu.
“Sio kwamba nawapa presha wachezaji ila tunatengeneza mazingira ya wao kufanya vizuri kama tungekuwa hatuna pesa ya kuandaa timu wachezaji wasingekuwa na moyo wa kujituma lakini sasa tunazo”>>>Amaju Pinnick
“Tumewapatia kila kitu kinachohitaji sasa wao wanachotakiwa ni kufanya vizuri mfano tumekubaliana kama watafika fainali na kutwaa Ubingwa basi pesa ya Ubingwa itagawanywa asilimia 50 kwa wachezaji na asilimia 50 inayobaki kwa chama cha soka NFF”>>> Amaju Pinnick
Michuano ya Kombe la Dunia 2018 itafanyika Urusi kuanzia June 14 hadi July 15 na Taifa litakaloibuka Bingwa litapata dola milioni 48, hivyo asilimia 50 ya hizo ni dola milioni ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 54 ndio watakazopewa wachezaji wa Nigeria kama watatwaa Ubingwa.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao