Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League umechezwa katika uwanja wa Anfield jijini Liverpool kwa kuzikutanisha timu za Liverpool dhidi ya wageni wao AS Roma ya Italia.
Liverpool ambao hawajacheza hata ya nusu fainali ya UEFA Champions League toka 2008 wamefanikiwa kuanza vyema safari ya kuelekea fainali baada ya kufanikiwa kuifunga AS Roma kwa magoli 5-2, Mohamed Salah Roberto Firmino ndio wamehusika kuimaliza AS Roma.
Mohamed Salah amefanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 35 na 45 na kutoa pasi mbili za magoli kama ilivyokuwa kwa Roberto Firmino pia aliyefunga magoli mawili dakika ya 61 na 68 sambamba na kutoa pasi mbili za magoli huku Sadio Mane akifunga goli la tatu dakika ya 56.
Magoli ya AS Roma yalipatikana dakika za lala salama 81 kupitia kwa Eden Dzeko kabla ya dakika nne baadae Diego Perotti kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati, kwa matokeo hayo Roma katika mchezo wa marudiano watahitaji ushindi wa magoli 3-0 ili waitoe Liverpool wakati Liverpool wao wakihitaji sare au kufungwa chini ya magoli matatu.
Mohamed Salah baada ya kufunga magoli mawili leo anakuwa ndio mchezaji aliyefunga magoli mengi kwa msimu (43) katika wachezaji wa Ligi tano kubwa Ulaya akifuatiwa na Ronaldo (42), Salah anakuwa mchezaji wa kwanza kutokea EPL kuwahi kufunga magoli 43 kwa msimu mashindano yote katika msimu mmoja baada ya Ruud van Nisterooy afanye hivyo (44) msimu wa 2003/4 akiwa na Man United.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao