Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayecheza soka katika club ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ameonekana kukubali uwezo wa kinda wa Man United Marcus Rashford.
Ronaldo amedhihirisha hilo kwa kuamua kumtumia zawadi Marcus Rashford yenye ujumbe wa kumtia moyo aendelee kufanya kazi katika soka anayoendelea kuifanya.
Cristiano Ronaldo amemtumia Rashford zawdi ya jezi namba 7 ya Real Madrid ambayo huvaliwa na yeye mwenyewe Ronaldo na kuiandika “Keep up the good work” akiwa ma maana “endelea kufanya kazi nzuri”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri kabla ya Ronaldo kujiunga na Real Madrid ya Hispania aliwahi kuichezea Man United kuanzia 2003 hadi 2009 alipoamua kujiunga na Real Madrid lakini ameendelea kuwa mahusiano mazuri na viongozi ma wachezaji wa Man United.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao