Shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia Bodi ya Ligi ambao ndio wasimamizi na waendeshaji wa Ligi Kuu Vodacom, leo imetangaza adhabu mbalimbali baada ya kamati ya saa 72 kukaa na kujadili matukio mbalimbali yaliokuwa yamejitokeza katika michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Tanzania bara.
Simba wao wamepigwa faini ya Tsh 500,000 kwa kosa la kuonesha vitendo vya kishirikina katika game dhidi ya Njombe Mji, kutokana na shabiki wao kuingia uwanjani kutoa taulo la kipa wa Njombe Mji, faini ya Tsh 500,000 pia kutokana na mashabiki wake kuingia uwanjani mwisho wa mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa Sugar, hivyo Simba jumla imepigwa faini ya Tsh milioni moja.
Pamoja na hayo pia club ya Simba imepewa onyo kali kutokana na kikosi chake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 6 wakati wa game ya Simba dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam iliyofanyika April 12 2018, hata hivyo Tafadwadzwa Kutinyu wa Singida United amefungiwa mechi tatu kwa kosa na faini ya Tsh 500,000 kwa kosa la kutupa taulo la kipa wa Mtibwa Sugar kitendo ambacho kinaashiria imani za kishirikina.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao