Siku moja baada ya nusu fainali za kwanza za UEFA Champions League kuchezwa, usiku wa April 26 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia nusu fainali mbili za UEFA Europa League kati ya Arsenal wakiikaribisha Atletico Madrid katika uwanja wa Emirates wakati Olympique Marseille walikuwa wenyeji wa FC Salzburg.
Arsenal wameshindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1, Arsenal walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 61 kupitia kwa Alexandre Lacazette lakini Atletico walifanikiwa kusawazisha goli hilo dakika 9 kabla ya game kuisha kupitia kwa Antoine Griezmann.
Kwa matokeo hayo sasa Arsenal game ya marudiano katika uwanja wa Wanda Metropolitano watalazimika kuhakisha wanapata ushindi au sare ya kuanzia goli 1-0 na kuendelea, wakati upande wa Marseille wao wamefanikiwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kupata ushindi wa magoli 2-0, hivyo mchezo wa marudiano wanahitaji sare tu kupita au wapoteze kwa chini ya goli 1-0.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao