Leo April 27, 2018 Naibu Waziri wa Kilimo, Dr. Mary Mwanjelwa, ameagiza wakulima wa korosho mkoani Lindi kupatiwa elimu namna ya kupambana na kuzuia ugonjwa wa mnyauko fusari ulioukumba zao hilo.
Ugonjwa huo unatokana na fangasi waliopo ndani ya udongo ambao hushambulia mikorosho kwa kasi kubwa, hali inayosababisha majani hubadilika kutoka rangi ya kijani na kuwa njano au kahawia kisha kukauka.
Akizungumza na wakulima katika Kijiji cha Legezamwendo Kata ya Liwale ‘B’ baada ya kutembelea kijiji hicho, Dr. Mary amesema, wakulima wanapoona dalili hizo wanapaswa kutumia njia ya dharura kwa kukata na panga mkorosho ulioathirika kisha kuchoma moto kifaa hicho.
Amesema tatizo hilo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi mapema kabla ya athari kubwa kujitokeza katika maeneo mengine.
“Ugonjwa huu ni hatari kwa zao letu kwani linarudisha nyuma uchumi wa serikali, lakini pia kwetu sisi wakulima kutokana uchumi wetu mkubwa sisi wakulima ni kilimo,” amesema Mwanjelwa.
BREAKING: RAIS MAGUFULI ALIVYOIPANDISHA HADHI DODOMA KUWA JIJI