Leo April 27, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wote waliohusika katika ulaji wa fedha BILIONI 2 za mradi wa maji wa Ntomoko.
Rais Magufuli amesema hayo wakati akifungua barabara ya lami kutoka Dodoma hadi Babati, Manyara yenye urefu wa Kilometa 251 ambayo imegharimu Bilioni 378.
“Mradi wa Maji wa Ntomoko ambao umeanza Miaka ya 80 mpaka leo 2018 mradi haujakamilika, miradi inayokuja mwaka huu imekamilika lakini huu wa Ntomoko unatomokea tu huko, inawezekana wahusika wapo, walikula BILIONI 2,” amesema Rais Magufuli
Ndipo Rais Magufuli akatoa maagizo “Vyombo vya dola na Wizara ya Maji iwatafute waliokula BILIONI 2 washughulikiwe, hatuwezi kubembelezana, Waziri wa Maji, PCCB, Polisi, muwatafute hawa, warudishe pesa zetu au wamalizie mradi wa maji”