Jumapili ya April 29 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam utachezwa mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga ambao kwa sasa kila mmoja anajitihada za kuhakikisha wanatwaa Ubingwa wa Ligi hiyo.
Yanga wanajiandaa kutetea taji lako hilo lakini Simba nao wanapanga kumaliza ukamewa vikombe Msimbazi, kuelekea game hiyo afisa habari wa Simba Haji Manara ameongea na waandishi wa habari na kuelezea kuhusiana na utimamu wa kikosi chake na hakina majeruhi.
Kubwa Manara amewaonywa watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kutowaitsa Simba na Yanga kuwa ni mahasimu bali hao ni wapinzani na watani wa jadi lakini neno mahasimu sio zuri kutumia kwani linaleta chuki kati ya mashabiki wa timu hizo.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao