Leo April 28, 2018 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wameongea na waandishi wa habari kuhusu huduma ya upandikizaji wa Figo kwa wagonjwa na hali ya mgonjwa aliyepandikizwa figo mwishoni mwa mwaka jana Prisca ambaye yupo mkoani Morogoro.
Akizungumza Dr. Jackline Shoo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Figo hospitali ya Taifa Muhimbili amesema wamepandikiza wagonjwa wanne kwa mpigo na wao wanaweza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi zaidi nchini.