Leo April 28, 2018 Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa amewataka Wakulima wa zao la Korosho mkoani Pwani, kuacha tabia ya kuuza korosho ambazo hazijakauka vizuri na kwamba kufanya hivyo kunapunguza thamani ya zao hilo kwenye soko.
Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa katika ziara yake ya kutembelea mikoa inayolima zao la Korosho, ambayo imekubwa na ugonjwa wa Mnyauko Fusari wa korosho, ametembelea mashamba ya korosho ambayo yameathiriwa na huo na kujionea hali ilivyo na baadaye akazungumza na wananchi ambapo amewataka wakulima kuacha tabia ya kuuza korosho ambazo bado hazijakauka.
ABBAS KANDORO AMEFARIKI, ALIKUWA RC DSM, MBEYA
BREAKING: Gari ya Polisi yagongana na Noah yenye askari wa JWTZ, wawili wafariki