Leo May 1, 2018 Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa ameagiza, kuchunguzwa kwa mchakato wa ujenzi wa ghala la korosho Kipalang’anda lililopo Mkuranga mkoani Pwani, ambalo limejengwa kwenye mkondo wa maji kwa thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5
Dr. Mwanjelwa amesema “Nimekuja kukagua ghala sababu mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga ina matatizo ya kutokuwa na maghala rasmi ndo maana hata korosho inakuwa haina ubora, sababu hamna maghala rasmi, mnatunza kwenye maghala madogo madogo”
“Pesa inayotumika hapa Bilioni 5. 6 ni pesa ya Serikali, tunawezaje kuweka ghala kwenye mkondo wa maji, kama DC, Mkurugenzi, Diwani, Mwenyekiti wa CCM upo hapa hamna taarifa na mradi umejengwa kwenye mkondo wa maji, naagiza uchunguzi wa haraka ufanyike” -Dr. Mary Mwanjelwa
MAGAZETI LIVE: Mabilioni yayeyuka, Lissu Nimesahau kutembea, Kigezo kipya Mikopo Vyuo Vikuu