Baada ya Rais Magufuli kutangaza kwamba hataongeza mshahara kwa wafanyakazi, Mbunge wa Mbinga mjini Sixtus Mapunda pamoja na Mbunge wa Singida mjini Mussa Sima walisimama Bungeni Dodoma leo May 2, 2018 na kuomba mwongozo wa kuitaka Serikali kutoa majibu ni lini itawaongezea mishahara wafanyakazi ambao hivi sasa wana hali mbaya kiuchumi.
Majibu ya mwongozo Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge akatolea ufafanuzi kwa kusema…>>>”Jana Rais alisema kuwa kwa sasa Serikali yake haiwezi ikaongeza mshahara lakini hali itakaporuhusu ataongeza kikweli kweli… sasa ni lini? Hadi hali ya uchumi itakaporuhusu ”
Bashe kazitaja sababu za elimu ya Tanzania kushuka viwango