Mbunge wa viti maalum Singida kupitia tiketi ya CHADEMA Jesca Kishoa amelieleza Bunge kuwa elimu ya Tanzania inapitia katika kipindi kigumu kwa Serikali kushindwa kuwekeza mipango mikakati ya kujitosheleza katika sekta hiyo.
“Elimu yetu inapitia kipindi kigumu sana, na hili limethibitishwa hata na marais waliopita akiwemo Kikwete. Tusiitazame elimu katika sura ya kutoa ajira peke yake isipokuwa tuitizame elimu katika sura pana hasa sura ya kiuchumi” –Jesca Kishoa
“Nchi zote ambazo ni magwiji kiuchumi kwanza waliwekeza katika sekta ya elimu, elimu ndio inashikilia uchumi wa dunia kwa sasa. Mfano wmepesi ni nchi ya China” –Jesca Kishoa
Bashe kazitaja sababu za elimu ya Tanzania kushuka viwango