Leo May 2, 2018 Upelelezi kesi inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari kuhusu kesi ya kumshambulia aliyekuwa Mtendaji wa kata ya Makiba, Neeman Ngudu ya mwaka 2014 umekamilika.
February 6 2018, Nassari alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru na kusomewa mashtaka ya kesi anayodaiwa kuifanya 2014 katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Jasmin Abdul ameahirisha kesi hadi June 6, 2018 ambapo mtuhumiwa atasomewa maelezo ya awali baada ya upande wa Jamhuri kusema upelelezi umekamilika.
RIPOTI YA CAG: ‘Msajili alimleta Lipumba kavamia Ofisi’ -CUF