Leo May 2, 2018 Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga ali-post picha ambayo aliweka caption inayosema “Nikizindua chanjo ya Kansa ya mlango wa kizazi wilayani Ulanga”.
Baada ya picha ya Mbunge Mlinga kusambaa, kupitia ukurasa wake wa Twitter Waziri wa Afya, Ummy Mwalim amesema kitendo hicho si sahihi na tayari ameshatoa maagizo Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Namnukuu alichoandika Twitter “Hii sio sahihi. Tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuu Afya kutoa maelekezo mara moja kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusisitiza uzingatiwaji wa Miongozo ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini. masuala ya kitaalamu yafanywe na Wataalamu.”
Hii sio sahihi. Tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuu Afya kutoa maelekezo mara moja kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusisitiza uzingatiwaji wa Miongozo ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini. masuala ya kitaalamu yafanywe na Wataalamu. https://t.co/8m436lDPyU
— Ummy Mwalimu (@umwalimu) May 2, 2018
KANISA KATOLIKI ARUSHA: Marufuku Bibi Harusi Mjamzito kuvaa Shela