Usiku wa May 2 2018 mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya UEFA Champions League kati ya AS Roma dhidi ya Liverpool ulichezwa nchini Italia, Roma ambao ni wenyeji waliingia uwanjani wakiwa tayari nyuma kwa magoli 5-2 waliyofungwa katika mchezo wa kwanza uliyochezwa Anfield wiki moja iliyopita.
Hivyo leo AS Roma waliingia kusaka ushindi kwa hali na mali na kuhakikisha wanasonga mbele, bahati haikuwa yao licha ya kuwa nyumbani na kuwa na mtaji mkubwa wa mashabiki AS Roma wameambulia rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Liverpool Champions League msimu huu baada ya kuifunga magoli 4-2 ila matokeo ya jumla yameondoa kwa tofauti ya goli moja 7-6.
Magoli ya AS Roma leo yamefungwa la kwanza James Milner wa Liverpool alijifunga dakika ya 15, Eden Dzeko dakika ya 52 na Radja Nainggolan aliyefunga magoli mawili dakika ya 86 na 94 kwa mkwaju wa penati wakati magoli ya Liverpool yalifungwa na Sadio Mane dakika ya 9 na Georginio Wijnaldum dakika ya 26 ya mchezo.
Pamoja na game hiyo kumalizika na Liverpool kupata nafasi ya kucheza fainali na Real Madrid May 26 2018 katika jiji la Kyiv nchini Ukraine katika uwanja wa Olimpiyskiy, mchezo huo unaacha rekodi ya kuwa ni mchezo pili wa Champions League wa mtoano nyumbani na ugenini kuzalisha magoli zaidi ya 12 baada ya ule wa Bayern vs Sporting (12-1) msimu wa 2008/9, huku kocha wao Jurgen Klopp akiwa kocha wa nne wa Liverpool kuwahi kuifikisha fainali ya UEFA baada ya Bob Paisley (3), Joe Fagan (2) na Rafael Benitez (2).
VIDEO: Sadio Mane ameipeleka Bongofleva katika dressing room ya Liverpool