Leo May 3, 2018 Viongozi wa Mkoa wa Iringa wamemshukuru Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali Mkoani humo na wameahidi kuendelea kumuungano mkono na kumuombea katika majukumu mazito anayoyatekeleza.
Viongozi hao waliojumuisha Waheshimiwa Madiwani, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na viongozi wa kimila wametoa shukrani hizo katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Rais Magufuli na kufanyika katika Ikulu ndogo Mjini Iringa.
Nakusogezea alichozungumza Mbunge wa Iringa wa Mjini Peter Msigwa mbele ya JPM. Rais umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa wewe hujali mambo ya vyama, na hii imedhirika kuwa kweli hujali vyama,”
“Umesaidia sana, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi, kama alivyosema Mahiga, kuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais, umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu Shilingi Bilioni 3.5,” amesema Msigwa
“Tuna stendi nzuri ipo Ipogolo ya karibu Shilingi Bilioni 3, tuna maji, kwa hiyo kuna vitu vimefanyika kwa kweli Mhe. Rais hupendelei, hela zinakuja hata sisi ambao ni wa CHADEMA unaleta hela, kwa hiyo tunakupongeza sana” -Msigwa
“Hii sio sahihi, masuala ya kitaalamu yafanywe na Wataalamu’ -Waziri Ummy