Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa onyo kwa mamlaka ya mapato nchini TRA kuacha kutumia nguvu na lugha chafu kwa wafanyabiashara wakati wa kukusanya kodi na endapo matukio hayo yakijitokeza wananchi wanaweza kwenda kutoa malalamiko kwa Wakuu wa mikoa na wilaya ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika.
Waziri mkuu amesema…>>>“Tunajua kwambani ni wajibu wa kila mtu kulipa kodi kwa kadiri ya shughuli zake za kuzalisha mapato zilivyo, tumeielekeza mamlaka ya TRA ihakikishe inapokwenda kukusanya kodi haitumii nguvu katika kukusanya kodi na hakuna sababu ya kumlazimisha”
MJADALA WA NYONGEZA YA MISHAHARA BUNGENI MAY 2 2018