Kampuni ya mtandao wa Twitter imewaambia watumiaji wa mtandao huo ambao ni takriban milioni 330 duniani kote kubadilisha password zao baada ‘kirusi’ kuingia kwenye mfumo wa mtandao huo na kusababisha password za watumiaji kuonekana kwa maandishi.
Kampuni hiyo imeeleza kuwa hakuna madhara yaliyofanyika kwani hakuna taarifa za watu zilizoibwa kutokana na kuonekana kwa password hizo, lakini ni vyema wazibadilishe kwa tahadhari.
Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Mkuu wa Twitter Jack Dorsey kwa kuandika kwenye account yake ya mtandao huo na kuomba radhi kwa kilichotokea.
“Hali ni mbaya sana ndugu zangu, wanavamia usiku”-Hasna Mwilima