Mbunge wa viti maalum CCM Lucy Mayenga alisimama Bungeni kuchangia mapendekezo yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo alionesha kukerwa na baadhi ya Wapinzania ambao wamekuwa wakilikosoa Jeshi la Polisi nchini kwamba limeshindwa kufanya kazi zao na kuitwa wapigadebe wa CCM.
Lucy Mayenga amesema…>>>“Watu walizoea kudeka, kuropoka mambo ya ajabu kila siku sasa lazima ifike wakati tushikishwe adabu, Nchi lazima ifike wakati itawalike. Watu wamefikia kusema kwamba Jeshi la polisi ni wapigadebe wa CCM”
“Sasa hivi watu wameshikwa pabaya, watumishi hewa na mafisadi wote wameshikwa pabaya kwahiyo tujue kwamba vita hii ni kubwa kuliko tunavyoweza kuifikiria” –Lucy Mayenga
Bashe kazitaja sababu za elimu ya Tanzania kushuka viwango