Kati ya fursa muhimu kwa wananchi wa Dodoma ni kusajliwa Vitambulisho vya Taifa kama sehemu ya maandalizi msingi ya kunufaika na kazi zitakazopatikana baada ya Mkoa huo kupandishwa hadhi na kuwa Jiji. Kati ya fursa muhimu ni pamoja na fusra za kibiashara, ubia katika uwekezaji ambazo zote hizi zinamlenga mtanzania.
Mambo yote hayo yamebainika wakati wa kutembelea na kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ikiwemo wilaya ya Dodoma.
Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo Afisa Usajili Mkoa wa Dodoma Khalid Marisho amesema mpaka sasa mwitikio wa wananchi ni mkubwa kulinganisha na hapo awali kabla wananchi hawajatambua na kuona manufaa ya kuwa na Kitambulisho cha Taifa.
Wananchi wa Kata ya Zuzu Wilaya ya Dodoma wameonyesha kufurahishwa na mwenendo wa zoezi hilo, baada ya kutambua manufaa makubwa yapatikanayo kwa mtu kuwa na Kitambulisho cha Taifa.
Mzee Ngowolo ni mkazi wa Zuzu mwenye umri wa miaka 65, ambaye amezungumza na kueleza kwanini amejitokeza kusajiliwai “Ni haki yetu ya Msingi sisi kutambuliwa kama Watanzania, mbali na kutambulika kirahisi kitambulisho kitaturahisishia katika upatikanaji wa huduma za kijamii kwani taarifa zote za muhimu zinazohitajika zitakuwepo kwenye Kitambulisho hicho”
Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa nchini inayoendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi zoezi ambalo linategemewa kumalizika kufikia mwishoni mwa mwezi May 2018.
Ayo TV MAGAZETI: Siri yafichuka, Wabunge wamuibua Akwilina