Utafiti kutoka barani Ulaya uliofanyika siku za hivi karibuni umegundua kuwa watu kutoka England na Wales wamepunguza kuhamahama kuanzia miaka 2000 ukulinganisha na miaka ya nyuma.
Inaelezwa kuwa hali ya kuhama nyumba kwa nyumba au eneo moja kwenda jingine, kwa wapangaji au hata wamiliki wa nyumba wenyewe ilikuwa kubwa sana miaka ya 1970.
Utafiti huu umefanywa na wataalamu wa masuala ya idadi ya watu kutoka Queen’s University Belfast kwa kuangalia matokeo ya sensa ya miaka takriban 40.
Mabadiliko haya yanatajwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la gharama ya makazi, mali na uhaba wa nyumba za gharama nafuu.
Agizo alilolitoa Waziri Ndalichako Bungeni “huo ni uhalifu”