Serikali ya Marekani imeahidi kutoa Dola Milioni 512 (sawa na Sh.Trilioni 1.17) kwa serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupambana na maradhi ya Ukimwi.
Akizungumza wakati wa kutoa ahadi hiyo, Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk.Inmi Patterson amesema fedha hizo zitatolewa kupitia mpango wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR).
Dk.Patterson amesema mpango huo unalenga kudhibiti janga la Ukimwi ifikapo September 2019.
“Serikali ya Marekani imetumia zaidi ya Sh.Trillion 10.26 kuzuia maambukizi ya Ukimwi nchini tangu 2004,” amesema.
Pia Patterson amesema matokeo ya utafiti wa viashiria vya Ukimwi Tanzania ya December 2017 yameonyesha ipo nyuma ya nchi nyingine za kikanda.
Naye Naibu Waziri wa Afya Dk.Faustine Ndungulile amesema wanashukuru kwa msaada wa fedha hizo, pamoja kuimarisha mikakati iliyopo ili kupambana na tatizo Ukimwi.
Dk. Ndungulile amesema miongoni mwa mikakati waliyonayo ni mpango wa watu kujipima wenyewe Ukimwi kwa njia ya mate.
Agizo alilolitoa Waziri Ndalichako Bungeni “huo ni uhalifu”