Mfanyakazi wa usafi katika nchi ya Korea Kusini ameokota vipande saba vya dhahabu katika jalala alilokuwa akisafisha na kupokonywa na jeshi la polisi.
Kulingana na gazeti la The Korea Times mfanyakazi huyo wa usafi alipata vipande saba vya dhahabu vyenye thamani ya mamilioni ya pesa alipokuwa akiondoa taka katika hoteli ya Incheon.
Polisi wanasema hawatamtunuku zawadi yoyote kwa kuwa ni kazi yake ya kusafisha na kuripoti vitu vilivyopotea.
Kupitia ukurasa wa twitter wa BBC Swahili wameuliza, ungefanyaje iwapo ungepata dhahabu kwenye taka?